INTRO
Mwishoni darasa la saba
Mimi na yeye ndio tulijuana
Sababu ya kukosa Ada
Mi kidato ikashindika
VERSE 1
Ndoto za udakitari
Kwisha habari
Zikapeperuka
Na yeye sekondari
Akaamishwa mbali
Mkoani Arusha
PRE-CHORUS
Hisia na balehe zilikutana kati
Mambo ya kupenda
Ujana maji ya moto
Eh moyo ngoja basi
Nikaja kusikia
Yuko gongo la mboto
Mara chuo Mtwara, Masasi
Nyie Wahenga waongo
Mambo ya dunia ndogo
Mbona sijui sasa yupo wapi
CHORUS
Namtafutaaa...
Bado namtafuta, mchumba wangu wa darasa la saba
Ajue sikuchezea fursa, ni wazazi walikosa ada
Bado namtafuta, mchumba wangu wa darasa la saba
Ajue sikuchezea fursa, ni wazazi walikosa ada
POST-CHORUS / REFRAIN
Tere liye, tere sanam
Tere liye, tere sanam
Tere liye, tere sanam
Tere liye, tere sanam
VERSE 2
Mara ya mwisho kumuona
Ni siku ya mahafali
Niliandika ujumbe ila hakuusoma
nyuma ya daftari
Suluhisho Mi kupona nijue angali
mzima yupo salama niache kusonona
Moyo upate afadhali
BRIDGE
Nikimuona nitamusimulia
Yote niliyoyapitia
Ajue yeye ndio chanzo cha Mimi kuishi Duniani
Nilivyommisi nitamkumbatia
Uenda naye kanimisi pia
Ni mawazo yanayonizunguka kichwani
VERSE 3 (REPEAT)
Ndoto za udakitari
Kwisha habari
Zikapeperuka
Na yeye sekondari
Akaamishwa mbali
Mkoani Arusha
PRE-CHORUS (REPEAT)
Hisia na balehe zilikutana kati
Mambo ya kupenda
Ujana maji ya moto
Eh moyo ngoja basi
Nikaja kusikia
Yuko gongo la mboto
Mara chuo Mtwara, Masasi
Nyie Wahenga waongo
Kwamba dunia ndogo
Mbona sijui sasa yupo wapi
CHORUS (FINAL)
Namtafutaaa...
Bado namtafuta, mchumba wangu wa darasa la saba
Ajue sikuchezea fursa, ni wazazi walikosa ada
Bado namtafuta, mchumba wangu wa darasa la saba
Ajue sikuchezea fursa, ni wazazi walikosa ada
OUTRO
Tere liye, tere sanam
Tere liye, tere sanam
Tere liye, tere sanam
Tere liye, tere sanam